Posts

Showing posts from February, 2021
Huku tukiendelea kumweka Mungu wetu kwanza tujikumbushe na kuzifuata njia rahisi (zenye gharama nafuu) za kupambana dhidi ya  COVID-19: 1.Tuvae barakoa Mara kwa Mara hasa   tunapokua maeneo yenye msongamano Wa watu wengi. 2.Tunawe Mara kwa Mara mikono yetu kwa Maji safi na tiririka au kutumia vitakasa mikono kabla na baada ya kugusa watu/maeneo yanayoweza kua sababu ya maambukizi ya COVID-19. 3.Tuzibe midomo yetu na kiwiko tukikohoa au kupiga chafya. 4.Tujitahidi kukaa umbali wa  angalau mita moja kutoka kwa mtu  mmoja hadi  mwingine tunapokua maeneo ya majumbani, makanisani/misikitini, benk, hospitalini shuleni nk. 5.Tule  mlo kamili kwani husaidia kuimarisha nguvu ya kinga  ya mwili katika kupambana dhidi ya magonjwa  mbalimbali  ikiwemo pia COVID-19. Kwa mfano. Ukipika ugali/wali kula na samaki/dagaa/nyama/maini/mayai/mbegu za mimea jamii ya mikunde kama maharage, kunde, njegere, njugu mawe nk.(kufuatana na bajeti yako kifedha), pia k...